Chapter 113
1 Haleluya. Enyi watumishi wa BWANA, sifuni, Lisifuni jina la BWANA.
2 Jina la BWANA lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
3 Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa.
4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5 Ni nani aliye mfano wa BWANA, Mungu wetu aketiye juu;
6 Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?
7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 Ili amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.
9 Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.
