Chapter 131
1 BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya Kifuani mwa mama yake; Roho yangu ni kama mtoto, Aliyeachishwa kunyonya.
3 Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.
